MDOGO WA MAFURU AFUNGUKA MANENO YA MWISHO ALIOAMBIWA KABLA YA KIFO CHA KAKA YAKE, UGONJWA WATAJWA

2024-11-11 35 0 17,168 YouTube

Download Convert to MP3

Wakati mwili aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya mipango, Lawrence Mafuru ukitarajiwa kuwasili nchini kesho Novemba 12, 2024, mdogo wa marehemu, Maira Mafuru amezungumza kauli ya mwisho ya kaka yake. Amesema, alizungumza na Mafuru Ijumaa iliyopita, siku moja kabla ya kifo chake kilichotokea Jumamosi ya Novemba 09, 2024 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Apollo nchini India. Akizungumza na Mwananchi nyumbani kwa marehemu, Maira alisema walizungumza kwa simu na kumwambia waendelee kumuombea, matibabu yake yakikamilika atarudi kuungana nasi tena. "Tulizungumza kwa simu, akasema atarudi salama matibabu yake yakikamilika, ilikuwa Ijumaa iliyopita," amesema. Akizungumzia kuondoka kwake, Maira amesema kifo chake kimewashtua kwani alikwenda akiwa katika Hali ya kawaida "Kama nilivyosema, aliondoka katika hali ya kawaida, anatembea mwenyewe, alituaga anakwenda kwenye matibabu ya kawaida, tuliamini ni matibabu ya kawaida, hata Ijumaa nilipozungumza naye alisema tumuombee atarudi salama matibabu yakikamilika," amesema Maira kwa huzuni. Akizungumzia makuzi ya Mafuru, amesema kaka yao huyo aliyekuwa wa kwanza kuzaliwa kati ya watoto wanne alikuwa ni kiungo muhimu kwenye familia.

coinpayu
Loading...